Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA), Prof. Maurice Mbago ametembelea mradi wa utanuzi na ukarabati wa shule nne za Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofadhiliwa na TEA na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliogharimu Sh. Bilioni 1.9
Katika ziara hiyo ya siku moja Prof. Mbago, ametembelea shule ya msingi Medeli na Kisasa ambazo ni miongoni mwa shule nne zilizofadhiliwa na TEA.
Shule nyingine zilizifadhiliwa ni Mlimwa C na Kizota.
Waalimu wakuu wa shule za Msingi Medeli Bi. Grace Lisasi na shule ya Msingi Kisasa Bi. Jesca Mwarabu wamesema mradi huo umesaidia kuongeza ufaulu na udahili wa wanafunzi
Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza TEA kwa ufadhili huo ambao amesema umeboresha mwonekano miundombinu na mandhari za shule nufaika
Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amehimiza wanufaika wa mradi huo kutunza vizuri miundombinu hiyo kwa manufaa ya
watanzania
Mfuko wa Elimu wa Taifa unaunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa kwa kufadhili ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo