MFUKO WA ELIMU WA TAIFA WABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA), Prof. Maurice Mbago ametembelea mradi wa utanuzi na ukarabati wa shule nne za Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofadhiliwa na TEA na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliogharimu Sh. Bilioni 1.9 Katika ziara hiyo ya siku moja Prof. Mbago, ametembelea shule ya msingi Medeli na Kisasa ambazo ni miongoni mwa shule nne zilizofadhiliwa na TEA. Shule nyingine zilizifadhiliwa ni Mlimwa C na Kizota. Waalimu wakuu wa shule za Msingi Medeli Bi. Grace Lisasi na shule ya Msingi Kisasa Bi. Jesca Mwarabu wamesema mradi huo umesaidia kuongeza ufaulu na udahili wa wanafunzi Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza TEA kwa ufadhili huo ambao amesema umeboresha mwonekano miundombinu na mandhari za shule nufaika Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amehimiza wanufaika wa mradi huo kutunza vizuri miundombinu hiyo kwa manufaa ya watanzania Mfuko wa Elimu wa Taifa unaunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa kwa kufadhili ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo