Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Kurugenzi ya Huduma za Taasisi

Kurugenzi ya Huduma za Taasisi

Jukumu kuu la Kurugenzi ni kusimamia na kuratibu shughuli za kifedha, kiutawala na kimkakati za Mamlaka kwa lengo la kuwezesha utekelezaji wa majukumu na kufikia malengo ya TEA. Kurugenzi hutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala ya fedha na uhasibu, rasilimali watu, mipango, ufuatiliaji na tathmini, pamoja na usimamizi wa vihatarishi.

Pia, kurugenzi ina jukumu la kuandaa mikakati inayohakikisha uzingatiaji wa viwango vya uhasibu na kanuni bora za usimamizi, kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani kwa ajili ya usalama wa fedha, na kuandaa taarifa sahihi za fedha. Aidha, inasimamia mikakati ya rasilimali watu, utendaji wa watumishi, mchakato wa mipango mkakati na bajeti, matumizi ya fedha za miradi, upatikanaji wa ukwasi wa kutosha, pamoja na utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa vihatarishi.  Kupitia majukumu hayo, Kurugenzi inahakikisha ufanisi wa kiutendaji, uimara wa kifedha na uzingatiaji wa matakwa ya kisheria na kiudhibiti katika utekelezaji wa shughuli za Mamlaka.

Kurugenzi ya Huduma za Shirika ina sehemu tatu (3):

  1. Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
  2. Sehemu ya Fedha na Uhasibu
  3. Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini