Kitengo cha Huduma za Sheria
Kazi kuu ya Kitengo cha Huduma za Sheria ni kutoa huduma na ushauri wa kisheria wa kina na wa kimkakati ili kuhakikisha Mamlaka inaendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazotumika. Majukumu haya yanajumuisha kuandaa mikakati, sera na taratibu za kisheria; kutoa ushauri wa kisheria kuhusu shughuli za Mamlaka; na kuhakikisha shughuli hizo zinaendana na matakwa ya sheria.
Kitengo husimamia nyaraka za kisheria, huandaa na kupitia mikataba, pamoja na kusimamia mashauri na uwakilishi wa Mamlaka katika masuala ya kisheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Solicitor General).
Aidha, Kitengo hutoa msaada wa kisheria na kiutawala kwa Bodi na Kamati zake kupitia majukumu yake kama Sekretarieti ya Bodi.
Kupitia majukumu haya, Kitengo cha Huduma za Sheria huhakikisha uadilifu wa kisheria wa Mamlaka, hupunguza vihatarishi vya kisheria na kusaidia katika kufanya maamuzi ya kimkakati.