Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Miradi ya STEM: Ushirikiano wa TEA na UNICEF-Tanza...

Miradi ya STEM: Ushirikiano wa TEA na UNICEF-Tanzania Kwa Ufadhili Wa Serikali ya Canada

13 Oct, 2026
Miradi ya STEM: Ushirikiano wa TEA na UNICEF-Tanzania Kwa Ufadhili Wa Serikali ya Canada

Tanzania  chini ya ufadhili wa Serikali ya Canada, imetekeleza miradi ya ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa maabara za sayansi katika shule za sekondari za katika mikoa ya Kigoma, Songwe na Tabora kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi, Teknolojia STEM.
Katika mwaka wa fedha 2023/2024, kiasi cha Shilingi milioni 344.2 kilitumika kuboresha maabara tisa, huku katika mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha Shilingi  milioni 936.7 kikielekezwa katika vyumba 44 vya maabara katika shule 20.
Miradi hiyo imeleta manufaa mbalimbali, yakiwemo kuongezeka kwa hamasa ya wanafunzi kuchagua masomo ya sayansi, kuimarika kwa ujifunzaji wa vitendo na kuboreshwa kwa mazingira ya kufundishia. Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko, wanafunzi 58 wa kundi la kwanza la wahitimu walipata matokeo yaliyotajwa kuwa mazuri, huku shule za Itumba, Nkangamo na Kamagi zikieleza kuongezeka kwa mwitikio wa wanafunzi katika kuchagua masomo ya sayansi.
Aidha, wanafunzi wameeleza kuwa masomo ya STEM yanawapa fursa ya kutimiza ndoto zao za kitaaluma, kujiajiri na kuchangia maendeleo ya jamii.
Shule nyingine za Sekondari zilizonufaika na miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya STEM ni pamoja na Shule ya Sekondari Kashoza (Kakonko), Gwanumpu (Kakonko), Migezi (Kibondo), Rugenge (Kakonko), Busami (Kibondo), Nyamidaho (Kasulu), Nyakitonto (Kasulu) Mount Samba (Kibondo) Masanga (Kigoma) zilizoko Mkoani Kigoma.
Katika mkoa wa Tabora shule nyigine zilizonufaika ni pamoja na Dkt. J.P. Magufuli (Kaliua), Goweka (Uyui), Langwa (sikonge), Ngulu (Sikonge), Kizengi (Uyui), Pangale (Sikonge) na Usagali (Uyui). Kwa upande wa Songwe shule za sekondari zilizonufaika ni Bupigu (Ileje), Shiwinga na Ndugu zote za Mbozi.
Kwa ujumla, ushirikiano huu umechangia kuboresha miundombinu ya elimu ya sayansi na kuimarisha mazingira ya kujifunzia katika shule zilizofaidika, hatua inayolenga kukuza maarifa na ujuzi wa wanafunzi katika sayansi na teknolojia.

Miradi Mingine