Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 moja ya kipaumbele miradi itakayotekelezwa na TEA ni ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo, kwa lengo la kuwezesha shule za sekondari kukabiliana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na elimu ya sekondari kupitia mpango maalumu wa Makundi Mawili (double cohort).
Zaidi ya Shilingi bilioni 4.2 zimetengwa kwa ajili ya kunufaisha zaidi ya shule 40 ambazo zinatarajiwa kupokea makundi mawili ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari