Ndoto za wasichana wa Mkoa wa Songwe za kuwa wataalamu katika fani za sayansi, teknolojia, uhandisi na tiba zinaendelea kukua kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Sifael Mboma (15), mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe, Mbozi, anatamani kuwa mhandisi. Anasema masomo ya sayansi yanamvutia kwa kuwa yanahusiana na maisha ya kila siku na humwezesha mwanafunzi kutatua changamoto mbalimbali kupitia maarifa na majaribio ya vitendo.
Sifael anawahimiza wasichana wenzake kutokuogopa masomo ya sayansi, akisema wana uwezo wa kusoma na kufaulu iwapo wataweka bidii.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndugu, Bw. Cosmas Nzowa, amesema idadi ya wasichana wanaosoma masomo ya sayansi imeongezeka kutoka 70 hadi 158, huku wasichana wakiwa 100, sawa na asilimia 63.2 ya wanafunzi wa mkondo huo.
Amesema ongezeko hilo limechangiwa na kuboreshwa kwa mazingira ya kujifunzia, ikiwemo ukarabati wa maabara mbili za sayansi kupitia ufadhili wa UNICEF kwa kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Naye Mwalimu wa Sayansi katika Shule ya Sekondari Shiwinga, Bw. Remmy Manfred Mwakifuna, amesema ukarabati wa maabara umeboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia, na kuwawezesha wanafunzi kufanya majaribio kwa vitendo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Ibrahim Nelson Mgalle, ameishukuru TEA na UNICEF kwa kuwezesha maboresho hayo, akisema yatachangia kuongeza hamasa na ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya sayansi.
Maboresho hayo yanaendelea kutoa fursa kwa wasichana wa Songwe kujiamini katika masomo ya sayansi na kujenga msingi wa kutimiza ndoto zao za kitaalum
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...