Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Elimu Ya Amali Ya Michezo Yaanza Kunufaisha Chief...

Elimu Ya Amali Ya Michezo Yaanza Kunufaisha Chief Sarwatt Sekondari

01 Nov, 2026
Elimu Ya Amali Ya Michezo Yaanza Kunufaisha Chief Sarwatt Sekondari

Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepokea ruzuku ya Shilingi 181,020,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya michezo na ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, hatua inayolenga kukuza vipaji vya wanafunzi na kuboresha miundombinu ya michezo shuleni hapo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa uwanja huo, Msaidizi wa Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Suzana Raphael, ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kuendelea kutoa ruzuku zinazochangia utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuimarisha elimu na kukuza vipaji vya wanafunzi.

Naye Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu wa TEA, Bw. Masozi Nyirenda, amemtaka mkandarasi na wasimamizi wa mradi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili wanafunzi waanze kunufaika na uwekezaji huo.

Kwa upande wao, walimu wa shule hiyo wameishukuru Serikali na wadau waliochangia upatikanaji wa ruzuku hiyo, wakieleza kuwa uwekezaji huo utasaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo, hususan soka, pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kukuza ujuzi kwa vitendo.

#TEA #ElimuYaAmali #MichezoShuleni #KukuzaVipaji #ElimuTanzania #MaendeleoYaElimu