Shule ya Sekondari Mafiga, inayofundisha amali ya kilimo, imepatiwa Sh 280,822,400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na mitambo ya kufundishia, ikiwemo trekta. Nayo Shule ya Sekondari Morogoro imepatiwa Sh 66,650,000 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na jukwaa la mpira wa pete. Kwa pamoja, miradi hiyo ina thamani ya Sh 347,472,400.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Msaidizi wa Kamishna wa Elimu kutoka WyEST, Bi. Suzana Raphael, aliipongeza TEA kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa na miundombinu inayosaidia utekelezaji wa mtaala wa elimu ya amali. Alisema Wizara itafanyia kazi changamoto zilizobainika ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu wa TEA, Bw. Masozi Nyirenda, alisema Mamlaka itaendelea kuunga mkono miradi ya elimu ya amali ili kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuongeza fursa za kujiajiri na kuajiriwa.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mafiga, Mwalimu Robert Marwa, aliishukuru Serikali kupitia WyEST na TEA kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kilimo, akieleza kuwa vinaboresha mafunzo ya vitendo. Naye Mwalimu Hussein Hussein alisema elimu ya amali imeongeza mwamko miongoni mwa wanafunzi na wazazi, huku vifaa vilivyopatikana vikitarajiwa kusaidia kuandaa wataalamu wenye ujuzi wa vitendo.
Miradi hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha elimu inayozingatia ujuzi na mahitaji ya soko la ajira, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inashiriki katika Maonyesho ya Tano ya Kitaifa y...