Benki ya NMB imepeleka tabasamu na matumaini katika shule tatu za msingi nchini baada ya kutoa vitimwendo (wheelchair) 30 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, hatua inayowawezesha kushiriki kikamilifu katika masomo na kuboresha upatikanaji wa elimu jumuishi.
Mchango huo, wenye thamani ya Sh.milioni 6.5, umetolewa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kupitia Mpango wa Uwajibikaji wa Kijamii wa Makampuni (CSR), unaolenga kusaidia shule na wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Msaada huo umeelekezwa katika shule ya msingi ya Salvation Army Primary – Dar es Salaam, Shule ya Msingi Katumba II – Mbeya na Shule ya Msingi Kilindoni ya Mafia, kila moja ikipata viti 10.
Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi wa Utafutaji Raslimali na Miradi ya Elimu, Bw. Masozi Nyirenda amesema mchango huu unaongeza upatikanaji wa elimu kwa usawa na kuwawezesha wanafunzi wenye ulemavu kuwa na mazingira wezeshi.
Mchango wa NMB Bank umeonesha jinsi taasisi za kifedha zinavyoweza kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuboresha elimu jumuishi nchini, huku wakitoa fursa sawa kwa kila mwanafunzi kujifunza katika mazingira bora na salama
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Elimu Na. 8 ya mwaka 2001, imepewa jukumu la kuhamasisha michango na kuratibu shughuli za Uwajibikaji wa Kijamii wa Makampuni (CSR) kutoka kwa taasisi za umma, mashirika binafsi na wafadhili wanaojitolea. Michango hiyo hutolewa kwa njia ya fedha, vifaa, au msaada wa aina nyingine na hutumika kwa ufanisi katika kutatua mahitaji ya elimu, kwa kuzingatia ubora, usawa na upatikanaji wa elimu.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...