Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, imefadhili ujenzi wa nyumba sita za walimu katika Shule ya Sekondari Ghasuma, iliyopo Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 258.
Mradi huo unalenga kuwawezesha walimu sita na familia zao kupata makazi bora na salama yaliyo karibu na shule. Uboreshaji wa makazi ya walimu unatarajiwa kuongeza urahisi wa upatikanaji wao shuleni na kuchangia kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa manufaa ya wanafunzi.
Kupitia miradi kama hii, TEA inaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu na kuchangia juhudi za Serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia nchini.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...