Miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu inayofadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imechangia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, hususan kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kikao na Mkurugenzi wa Rasilimali na Usimamizi wa Miradi, Zacharia P. Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, alitoa pongezi kwa TEA kwa mchango wake katika kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto katika jimbo hilo.
Mhe. Issaay, akiwa pamoja na Mbunge wa Mbulu Vijijini, Emmanuel Nuwas, alisema miradi ya TEA imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha elimu, hususan kwa watoto wa kike waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...