Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
TEA Yashiriki Maonyesho Ya Tano Ya Kitaifa Ya Sido...

TEA Yashiriki Maonyesho Ya Tano Ya Kitaifa Ya Sido Kahama

23 Oct, 2026
TEA Yashiriki Maonyesho Ya Tano Ya Kitaifa Ya Sido Kahama

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inashiriki katika Maonyesho ya Tano ya Kitaifa ya Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Magufuli, Kahama, mkoani Shinyanga.

Maonyesho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Teknolojia na Soko: Chachu ya Viwanda Vidogo.” Kupitia maonyesho hayo, TEA inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma, programu na fursa za ufadhili zinazotolewa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa elimu na mafunzo ya ujuzi nchini.

Ushiriki wa TEA katika maonyesho hayo unatokana na jukumu lake la kusimamia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi, unaolenga kuwawezesha vijana na wanawake kupata mafunzo ya ujuzi yanayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa, ikiwemo katika sekta ya viwanda vidogo. Kupitia mfuko huo, maelfu ya wanufaika wamepata fursa ya kujifunza ujuzi mbalimbali unaochangia kuboresha maisha yao na kukuza shughuli za kiuchumi.

TEA inakaribisha wananchi kutembelea banda lake ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma na fursa zinazotolewa na Mamlaka katika kuendeleza elimu, mafunzo ya ujuzi na kujenga uwezo wa wananchi nchini Tanzania.